Jifunze ujasiriamali

Jinsi ya kutambua mawazo ya biashara katika mazingira unayoishi



Katika pitapita za blog hii ilikutana na tangazo ndani ya basi la daladala iliyokuwa imeandikwa “hata mbuyu ulianza kama mchicha” ni kweli hata wazee walikuwa watoto. Na ni ukweli usiopingika kuwa biashara kubwa kubwa tunazozishuhudia hazijashushwa kwa njia za mazingaombwe.

Wafanya biashara maarufu kila mmoja ana historia iliyomfikisha katika mafanikio aliyofikia. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, na wengine wengi hawakuoteshwa kuwa na mafanikio waliyonayo, bila kuwa na mwanzo uliowafikisha hapo walipo.  

Fursa na mawazo mbalimbali ya biashara yanatoka katika mazingira yanayotuzunguka; majumbani, makazini, mashuleni, safarini n.k  Wajasiriamali waliofanikiwa hupata mawazo ya kuanzisha biashara, kuwa makini na kulifanyia kazi wazo la biashara alilolivumbua katika mazingira yanayomzunguka.

Ni vema ukatoka nje kujichanganya na watu ili uone fursa mbalimbali zilizopo kwa muda huo ambazo zitaweza kukusaidia ukatoa maamuzi ya kuanzisha biashara yako huku ukikutana na wafanyabiashara waliotangulia kwa kuiga tabia za kisiriamali. Kuna usemi usemao“mvumbuzi sio tu kufumbua kitu bali ni uchakarikaji wa kutafuta fursa na mawazo sahihi ya kuanzishisha biashara”.

 Njia 3 za kuvumbua wazo sahihi la biashara

Kwa kujifunza kupitia kwa wengine wanaotuzunguka, utakutana na mawazo mbalimbali na ndio njia ya kupata majibu ya kukuwezesha kujua ni biashara gani uanzishe. Kuna njia tatu za kufuata:-

1.    Weka orodha ya mawazo yako

Hakuna biashara isiyolipa; utashangaa mtu mmoja anafungua biashara leo inakufa baada ya miezi sita. Lakini jirani yake ndani ya miezi sita anafungua na biashara nyingine ama kupanua maradufu biashara yake. Kila siku ongeza angalau fursa moja kwenye daftari lako. Usichague fursa; zote ni nzuri kama ukiwa na mipango na malengo.

Usikate tama, jiulize kwa nini hawa wameweza na kwa nini wewe ushindwe? Jipe moyo “hashindwi mtu hapa” Uhondo wa ngoma uingie ucheze mwenyewe. Na mara nyingine matatizo ndio hupelekea mtu kujikuta anaangukia kupata wazo sahihi la biashara.

2.    Toka nje, jichanganye na watu

Mawazo ya kibiashara hayapatikani kwa kukaa ndani na kusubiri wazo lishuke kutoka mbinguni. Unahitajika ubunifu ambao unaweza kuupata kupitia maonyesho ya biashara, kutembelea wafanyabiashara wazoefu na kubadilishana mawazo. Ikiwezekana “wawinde” wafanyabiashara unaowafahamu ambao unaweza kuongea kuhusu wazo lako. Ishi kwa kuangalia wanavyoendesha biashara zao. Wengi hukatisha watu tama, usiwajali.

3.    Iga mbinu za kupambana na changamoto

Matatizo yapo kila siku, kila sehemu, muda wowote. Biashara zote zina changamoto, jifunze ni jinsi gani wafanyabiashara wanavyopambana na changamoto zinazowazunguka na utapata njia muafaka ya kupambana na hivyo kuendelea na maisha. Iga na uweze kuzitumia mbinu hizo ila kuwa makini kiga mazuri huku ukiyaacha yale mabay

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UJASIRIAMALI