UJASIRIAMALI

Ugumu wa kupata Mitaji Wajasiriamali wamejikuta katika matatizo ya kubeba mizigo ya madeni kiasi cha kushindwa kuendelea Nini maana ya mtaji? Watu wengi wanaufahamu "Mtaji" kwa lugha rahisi kama "Kianzio" cha biashara. Ni kweli, kwa mfano mtaji wa mama Ntilie ni Maji, sufuria, jiko, mkaa, mwiko, sahani, pamoja na fedha ya kununulia chakula kama mchele, nyanya, maharage, chumvi n.k. Sasa basi katika mtiririko wa mahitaji yaliyotajwa hapo, vyote vinahitaji pesa ili kuvipata. Tatizo liko wapi? Kupata mtaji kwa nyakati hizi imekuwa jambo linalosumbua watu wengi. Mabenki yanasita kukopesha wafanya biashara wadogo sana (Micro businesses) kutokana na sababu kadha wa kadha ambazo kwayo ukiangalia zina uzito. Kada hii ya wafanya biashara huwa hawaaminiki kwa wakopaji wakubwa kama mabenki na taasisi za fedha kutokana na sababu zifuatazo: Hawana ofisi za kudumu; Wanakosa dhamana n.k Kupata fedha za kuanzisha biashara imekuwa ni kama ndoto!! ...